×
Admin 08-01-2024 Case Laws

Tarehe 28/10/2020 Kama Mnakumbuka ulikuwa Uchaguzi Mkuu Tanzania, Bahati Mbaya Tito na John Tulla walikosa haki ya kupiga kura kutokana na kuwa mahabusu, Tarehe 2/3/2023 walifungua kesi Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, kupinga wafungwa kutokupiga kura kwenye chaguzi za serikali.

Magoti na Tulla walifungua shauri hilo Mwaka 2022 dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Jeshi la Magereza.

Wakidai kuwa kifungu 11(1) (c) cha Sheria ya Taifa Uchaguzi kinachoweka zuio kwa wafungwa wanaotumikia adhabu ya kunyongwa na wanaotumikia adhabu ya kifungo cha kuanzia miezi sita.

kinakinzana na Katiba Ibara ya 5(1) ambayo inaeleza kuwa Kila raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 anayo haki ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.

Japokuwa kifungu hicho hakiweki zuio la utekelezaji haki hiyo kwa mahabusu wanaosubiri usikilizwaji wa kesi zao, lakini Jeshi la Magereza halijaweka utaratibu unaowawezesha wafungwa/Mahubusu kutekeleza haki yao ya msingi.

Jaji Luvanda katika uamuzi wake amekubaliana na hoja za Wakili Seka kwa niaba ya wadai kuwa kifungu hicho kuweka zuio hilo kwa wafungwa wote wanaotumikia adhabu kuanzia miezi sita kinakiuka Ibara ya 5(1) ya Katiba ya Nchi.

Kwa Upande wa wadaiwa wakati wa usikilizwaji walipinga madai hayo, wakisema kuwa NEC imekuwa ikiwawezesha raia wote kutekeleza haki hiyo kwa mujibu wa sheria. 

Jaji Luvanda Amesema kuwa haki ya kupiga kura ya mahabusu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ihifadhiwe na kulindwa na Katiba.

Pia Jaji Luvanda amesema kuwa ingawa Ibara ya 5(2), imesema kuwa Bunge linaweza kutunga sheria kuweka sharti la kuzuia raia wa Tanzania kutekeleza haki hiyo, lakini Bunge kwa kuweka sharti ya zuio kuzingatia kifungo limekwenda nje ya muktadha wa Ibara hiyo ya Katiba.

Amefafanua kuwa Bunge lingeweza kuorodhesha makosa makubwa ya jina ambayo mtu akitiwa hatiani anaondolewa haki hiyo kama vile makosa ya uhaini na mauaji ambayo adhabu yake ni kunyongwa. 

Hukumu ya Jaji Elinaza Luvanda, 22.12.20 Mahakama Kuu ilibatilisha kifungu cha 11(1)(c) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kilichoweka zuio la wafungwa kupiga kura. Hiyo ni kufuatia shauri la kikatiba la Tito Magoti na John Tulla

Submit Comment

Subscribe Us

Enter your email below to join our community of clients and legal professionals who trust us to provide valuable information straight to your inbox.