×
Admin 08-01-2024 Case Laws

Hii ni kesi maarufu ya jinai(kuua bila kikusudia kesi ya Mwaka 1969) Sultan aliua mtu akidhani ni nguruwe Pori, Bwana Sultan Maginga Alishtakiwa kwa kesi ya kumuua MTU kwa mkuki usiku wakati akilinda shamba lake, ulikuwa wakati wa Usiku Sultan alisikia kelele zikitoka kwenye shamba lake akihisi ni nguruwe kumbe in watu walikua wakifanya mapenzi shambani kwake.

Bwana sultan Maginga alikuwa akisumbuliwa sana  na nguruwe pori kwenye shamba lake, ambao walikuwa wanakula mazao yake aliamua kulinda shamba lake usiku dhidi ya hao nguruwe waharibifu.

Usiku mmoja sultan kama kawaida yake alielekea shambani kwake akiwa na mkuki tochi akaelekea shambani kwake kwenda kulinda baada kufika shambani kwake aliona kwenye vichaka vya shamba lake nyasi zikicheza cheza.

Akawasha tochi kuona ni nini kinaendelea lakini bahati mbaya tochi yake ilikuwa ina mwanga hafifu haukuweza kuonesha ni nini dhahiri kinaendelea au kama ni nguruwe wale waharibifu aliuliza kuna mtu hapo lakini hakupata majibu yoyote aliuliza tena mara ya pili lakini hakupata majibu.

Majani yasivyokuwa na siri bhana yalizidi kulalama bwana sultani maginga akaamua kurusha mkuki wake ambao ulimchoma vibaya sana mmoja wa wale watu pale shambani ambao walikuwa wanafanya mapenzi kwenye shamba la bwana sultan maginga.

Sultan alishatikiwa mahakamani kwa kesi ya mauaji lakini alijitetea kwamba aliuliza kabla ajarusha mkuki ni nani? na kulikuwa hakuna majibu yoyote kama kawaida akadhani ni nguruwe waharibifu Ndio maana akarusha mkuki kumpata huyo nguruwe Kumbe bahati mbaya walikuwa watu.

Mahakama ilisikiiza maelezo ya pande zote mbili na kuibua defence ya Mistake of Fact kwa bwana Maginga wakiamini Maginga aliua pasipo kukusudia kwani intention yake (Mens rea) haikua imelenga kuua MTU Bali alihisi anaua nguruwe.

Jaji aliishia kusema ushahidi ulioletwa mahakamani dhidi ya bwana sultani haujitoshelezi kumtia hatiani ni jambo la kawaida na kwakuwa aliuliza na hakusikia chochote kwahiyo kumtia hatiani ni vigumu.

Submit Comment

Subscribe Us

Enter your email below to join our community of clients and legal professionals who trust us to provide valuable information straight to your inbox.