×
Admin 08-01-2024 Case Laws

Kwa Wale watu ambao wamesahau kuhusu tukio hili, Daudi Mwangosi aliuawa Septemba 2, mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kazi.

Siku hiyo Chama cha demokrasia na Maendeleo walikuwa na Maandamano na Mkutano mkubwa kwa Pamoja katika kijiji cha nyololo, kwa ajili ya kufungua tawi la chama hicho.

Daudi Mwangosi alikuwa ni mmoja wa waandishi wa habari waliojitokeza kwenda kuchukua habari juu ya tukio hilo, hali ilibadilika kutoka  kutafuta habari akageuka yeye mwenyewe kuwa habari nzito iliyotikisa taarifa za vyombo vya habari za hapa nchini na nje ya mipaka ya nchi.

Daudi Mwangosi Mwandishi wa habari wa Channel Ten alipigwa bomu la machozi kwenye tumbo na askari aitwaye Pasificus Saimon na kufariki papo hapo.

Picha zilizochapishwa mtandaoni kipindi hiko, zilishotuua watu wengi na watu wengi walisema polisi walifanya kitendo hicho bila huruma na polisi kuficha ukweli wa mauaji hayo. 

Alhamisi ya Februari 6, 2015, Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ilianza kusikiliza kesi ya mauaji ya Daudi Mwangosi Dhidi ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Pacificus Cleofas Simon mwenye namba G 2573.

Katika mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Sunday Hyre, anadai kuwa Septemba 2, mwaka 2012, mtuhumiwa (Pacificus Cleofas Simon) alimuua Mwangosi kwa kumpiga kwa bomu kwa makusudi. Hata hivyo, mtuhumiwa alikataa shitaka hilo. 

Mtuhumiwa alitetewa  na Wakili Rwezaula Kaijage. Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Jaji Paulo Kihwelo, Baada ya Kusikiliza Ushahidi wa Pande zote Mbili 

Jaji Kihwelo Julai 25, katika Mahakama Kuu Ya Tanzania Kanda ya Iringa, alimtia hatiani kifungo cha miaka 15 Jela aliyekuwa Askari kikosi cha kutuliza ghasia Bw. Pacificus kwa mauaji ya kutokukusudia.

Lakini Askari huyo alikata Rufaa, na Mahakama ya rufaa ilitengua hatia aliyopewa askari huyo ya kifungo cha miaka 15 jela na kuitaka Mahakama kuu kanda ya iringa isikilize kesi hiyo upya.

Submit Comment

Subscribe Us

Enter your email below to join our community of clients and legal professionals who trust us to provide valuable information straight to your inbox.