Moja ya Kesi iliyotikisa Fani ya Sheria, katika utoaji Haki, ni Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tabora (2006) Bw. Ditopile Mzuzuri (60), kumpiga risasi dereva wa daladala, Bw. Hassan Mbonde (33) maeneo ya kawe jiji Dar es salaam.
Ditopile, alituhumiwa kumuua dereva huyo saa 2.30 usiku, njia panda ya barabara ya Kawe na Bagamoyo, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kuchukizwa na hatua ya gari lake (aina ya Prado) lilokuwa likiendeshwa na dereva wa Ditopile, Bw Nassoro Mohamed (42) kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.
Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.
Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.
Mashuhuda wa Tukio hilo wanasema wakati dereva wa Ditopile Bwana nasoro akiendelea kukagua gari, Ditopile naye alishuka kuungana na dereva wake kukagua uharibifu wa gari hilo, Ditopile alimfuata Marehemu(Dereva wa Daladala) na kumuamuru ashuke ili aangalie uharibifu aliofanya, na waende polisi, Lakini marehemu alimueleza ditopile amsamehe maana ajali hiyo imetokea bahati mbaya
Bahati Mbaya Ditopile hakukubaliana Msamaha huo na kuendelea kumwambia dereva(Marehemu) ashuke na kumwambia maneno hayo ataeleza polisi, Mashuhuda wanasema Marehemu alipoona ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali alifunga kioo cha gari ili kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo
Jambo hili lilimkwaza sana ditopile na kumfanya atoe bastola yake na kuanza kuitumia kugonga kioo cha gari hiyo huku akimsisitiza ashuke kwenye gari hiyo hata hivyo mashuhuda wanasema marehemu aligoma kutii amri ndipo Ditopile alifyatua risasi iliyopenya kwenye kioo cha gari na kufumua kichwa cha Marehemu.
Upelelezi wa kesi dhidi ya Ditopile ulichukua miezi minne tu hadi mashitaka kubadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya kutokusudia, Baada ya kesi kubadilishwa, Ditopile alitoka nje kwa dhamana.
Kesi ya mshitakiwa huyo ilisababisha mahabusu katika magereza ya Dar es Salaam na kwingineko, kugoma kuingia kwenye magari kwenda mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kesi zao, wakidai mahakama haijatenda haki na kutaka mtuhumiwa arudishwe Mahabusu, Mgomo huo wa siku tano haukuwahi kutokea nchini.
Hata hivyo, mwaka 2008 ikiwa bado kesi yake haijapata hukumu, kapteni Ditopile aliaga dunia katika hoteli ya Hilux mkoani Morogoro akiwa na mke Mdogo. Sababu ilitajwa kuwa mshtuko wa moyo.
Enter your email below to join our community of clients and legal professionals who trust us to provide valuable information straight to your inbox.