Mwaka 1993 Mchungaji Christopher Mtikila alifungua shauri la kikatiba Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma, kupinga sharti la mgombea wa uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa na akapewa ushindi wa mahakama kuu kutamka kifungu hiko ni batili.
Katika kesi hiyo Mchungaji mtikila aliomba mahakama kuu mambo mawili moja mahakama kuu itamke kifungu 39 na 67 cha katiba jamhuri ya muungano zilizorekebeshwa na sheria ya 8 kwa sheria namba 34 ya mwaka 1994 kwamba ni batili na ni kinyume cha katiba.
Pili aliomba Mahakama kuu itamke wazi kuwa kila mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa mujibu wa ibara 21 ya katiba bila kulazamishwa au kudhaminiwa na chama chochote cha siasa hivyo mtu yoyote anaweza kugombea kama mgombea binafsi.
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma chini ya majaji watatu Jaji Manento, Jaji Salim Masati, Jaji Thomas Mahayo wanayakubali mambo yote mawili ambayo MCh Mtikila aliomba mahakama kwa kutamka marekebisho 8 ya katiba ni batili, ibara 39 na 67 ni batili zifutwe katika vitabu vya sheria.
Lakini Serikali ilikata Rufaa na Mahakama hii ilibatilisha Hukumu ya Mahakama kuu hivyo inawapa ushindi Serikali na hapo jini mkata kamba alivyonajisi katiba yetu na kulinda ubatili.
Enter your email below to join our community of clients and legal professionals who trust us to provide valuable information straight to your inbox.